Hati hii ni sehemu ya mkataba kati yako na Deriv na inapaswa kusomwa pamoja na Masharti ya Jumla ya Matumizi kwa wateja (yanayojulikana kama "Masharti ya Jumla"). Maneno yoyote yaliyoelezwa katika masharti haya ya ziada yatazingatiwa kuwa na maana iliyotolewa katika Masharti ya Jumla.
1. Utangulizi
1.1. Masharti haya ya ziada yanatumika kwa wateja wote ambao wana akaunti na Deriv (BVI) Ltd.
1.2. Ikiwa kuna tofauti yoyote au upotofu kati ya masharti haya ya ziada na/au nyaraka zingine zozote zinazounda sehemu ya Makubaliano, masharti haya ya ziada yatapewa kipaumbele kuhusiana na akaunti yako na Deriv (BVI) Ltd.
1.3. Deriv (BVI) Ltd. ina leseni chini ya Sheria ya Biashara ya Usalama na Uwekezaji kufanya huduma za uwekezaji, na imeidhinishwa na kudhibitiwa na British Virgin Islands Financial Services Commission (“BVIFSC”).
2. Ushughulikiaji wa fedha zako
2.1. Tunaweza kutumia fedha zako kutimiza wajibu tulio nao katika kuweka mipaka ya hatarishi, kurekebisha, au kutatua biashara zako za derivatives.
2.2. Tunaweka fedha zako katika akaunti za benki ambazo ni tofauti na akaunti zetu za uendeshaji. Katika tukio la ufilisi, tuna mipangilio ya mkopo kati yetu na kampuni yetu mama ambayo daima, kwa kiwango fulani, itagharamia dhima yoyote inayodaiwa na wateja.
3. Utekelezaji wa oda
3.1. Kwa mujibu wa masharti ya leseni yetu, sisi tutakuwa washirika wa biashara yako. Tutaweza kuchukua jukumu la kuwa wakala kwa niaba yako tunapotekeleza maagizo yako, au kuwa kama mhusika mkuu, ambapo tutakuwa sehemu pekee ya utekelezaji wa biashara zako zote.
3.2. Wakati oda ya kununua au kuuza chombo inawekwa kwenye akaunti yako ya Deriv MT5, oda yako inaweza kupelekwa kwa mtoa ukwasi ambaye hutupatia huduma.
4. Maswali ya jumla
4.1. Ikiwa una maswali kuhusu akaunti yako ya biashara na Deriv (BVI) Ltd., unaweza kuwasiliana nasi kupitia Kituo chetu cha Msaada au kwa kuzungumza na mwakilishi kupitia mazungumzo mubashara.
4.2. Tumejizatiti kutatua swali lako kwa muda mfupi iwezekanavyo na tunathamini uvumilivu wako kwa kutupa muda wa kutatua jambo hilo.
4.3. Iwapo hatutaweza kutatua swali lako au unahisi majibu yetu hayaridhishi, unaweza kuwasilisha malalamiko rasmi kwetu kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika sehemu ya “Malalamiko” hapa chini.
5. Malalamiko
5.1. Ikiwa ungependa kuwasilisha malalamiko kuhusu Huduma zetu, unaweza kututumia maelezo yanayohusiana na malalamiko yako kupitia complaints@deriv.com. Tutachunguza maswali yako na tutakujibu rasmi ndani ya siku 15 za kazi kuanzia tarehe ambayo malalamiko yatapokelewa.
5.2. Iwapo malalamiko yako niya muhimu (tazama hapa chini) na hatujayatatua kwa kuridhisha ndani ya miezi 3 kuanzia tarehe ambayo malalamiko yako yatapokelewa, unaweza kuwasilisha malalamiko yako kwa BVIFSC.
5.3. Kulingana na Kifungu cha 69B(1) cha Kanuni za Udhibiti, malalamiko yanachukuliwa kuwa ya muhimu pale yanapodai mojawapo au zaidi ya yafuatayo:
5.3.1. Uvunjaji wa sheria au kanuni ya udhibiti;
5.3.2. Uovu wa makusudi, utovu wa maadili, au mwenendo usiofaa kwa upande wa mwenye leseni au mmoja wa wakurugenzi, wafanyakazi, au mawakala wake;
5.3.3. Kurudiwa au kujirudia kwa jambo ambalo tayari lilishalalamikiwa hapo awali (iwe ni la muhimu au vinginevyo); au
5.3.4. Kwamba mlalamikaji amepata, au huenda akapata, hasara ya kifedha ambayo ni kubwa kulingana na hali yake ya kifedha.