Deriv MT5 signals

Huduma ya biashara ya MT5 signals (ishara) inakuruhusu wewe kujisajili na kunakili biashara za wafanyabiashara wazoefu au kutoa mikakati yako kwa wafanyabiashara wengine kwa ada ya usajili.

Nakili biashara za wataalamu moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Deriv MT5 bure au kwa ada. Mara tu unapojisajili kupata signals (ishara) ya biashara, mikataba ya mtoa huduma itaigwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya biashara ya Deriv MT5 kila mara watakapo fanya biashara.

Faida za kujiandikisha kwenye ishara za biashara za MT5

Punguza hatari ya biashara kwa kunakili biashara kutoka kwa wafanyabiashara wabobevu.

Okoa muda – jisajili kupata ishara ili kufanya biashara otomatiki.

Rahisi kusanidi - hakuna usakinishaji unaohitajika.

Ufichuzi kamili wa utendaji wa kila mtoa huduma.

Hakuna magawio wala ada zinazofichwa.

Securing your trading account with verification codes, secure web browser and antivirus software protect your devices.

Jinsi ya kujisajili kupata (signal) ishara za biashara ya MT5

Hatua ya 1

Nenda kwenye MQL5 Signals

Katika kituo cha biashara yako ya MT5, nenda kwenye Zana na uchague MQL5 Signals.

Hatua ya 2

Jisajili kwa mtoa huduma za ishara

Chagua mtoa ishara unaependelea na bonyeza “Jisajili”.

Hatua ya 3

Maliza usajili wako

Panga vigezo vyako vya biashara na udhibiti wa hatari. Kisha bonyeza “SAWA” kukamilisha usajili.

Jinsi ya kurejesha au kughairi usajili wako

Hatua ya 1

Nenda kwenye Takwimu Zangu

Katika paneli ya Navigator, nenda kwenye Ishara na bonyeza ‘Takwimu Zangu’.

Hatua ya 2

Chagua mtoa huduma

Chagua mtoa huduma za signal (ishara) unayemtaka kuhuisha au kufuta usajili wako.

Hatua ya 3

Huisha au jiondoe

Bofya”Huisha” au “Jiondoe” ili kufufua au kughairi usajili wako.

Kumbuka:

  1. Akaunti ya jumuiya ya MQL5 inahitajika ili kujisajili kwa ishara za biashara. Ikiwa bado hauna akaunti, tembelea MQL5.com kujisajili.
  2. Ili kujisajili kupata (signals) ishara za kulipwa, weka fedha kwenye akaunti yako ya MQL5.
  3. Unaweza kujisajili kwa mtoa ishara mmoja tu na akaunti moja ya Deriv MT5 wakati wowote. Unaweza kutumia ishara yako kwenye kompyuta tatu tofauti.
  4. Mara tu umesajiliwa kupata ishara, hutokuwa na uwezo wa kufanya biashara mwenyewe kwa akaunti hiyo hiyo ya Deriv MT5.
Nenda kwenye Deriv MT5

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara mtaalamu, shiriki mikakati yako na wafanyabiashara wengine bure au kupitia mpango wa usajili. Wakati wafanyabiashara wanaposajili kupata ishara yako ya biashara, biashara zako zinaigwa moja kwa moja kwenye akaunti zao kila wakati unapoweka biashara.

Faida za kuwa mtoa ishara za biashara za MT5

Rahisi kusanidi - hakuna usakinishaji unaohitajika.

Kipato cha ziada kutokana na usajili wa kila mwezi.

Okoa muda – biashara zinaigwa moja kwa moja kwenye akaunti za wasajiliwa wako.

Securing your trading account with verification codes, secure web browser and antivirus software protect your devices.

Jinsi ya kuwa mtoa (signal) ishara za biashara

Hatua ya 1

Jisajili kama muuzaji

Ingiza kwenye akaunti yako ya MQL5. Katika ukurasa wa ishara, bonyeza ‘Jisajili’ na ufuate hizi hatua.

Hatua ya 2

Ongeza ishara

Bonyeza “Unda ishara” na kamilisha fomu kwa kutumia taarifa za akaunti yako ya Deriv MT5.

Hatua ya 3

Simamia ishara (signal)

Nenda sehemu ya ‘Ishara Zangu’ ili kusimamia ishara zako.

Kumbuka:

Unapounda ishara, ingiza yafuatayo kama jina la seva ya akaunti yako katika eneo la Broker kwenye fomu:

  1. Deriv-Demo ikiwa ishara yako ni kwa ajili ya akaunti za demo tu
  2. DerivSVG-Server au DerivSVG-Server-02 ikiwa ishara yako ni kwa ajili ya akaunti halisi tu. (Unaweza kupata jina la seva la akaunti yako kwenye dashibodi yako ya Deriv MT5.)
Nenda kwenye Deriv MT5

Maswali yako yamejibiwa